Home Sports YANGA HAO KUIBUKIA MALI KAMILIKAMILI

YANGA HAO KUIBUKIA MALI KAMILIKAMILI

BAADA ya kumaliza kete yao ya Ligi Kuu Bara Februari 22 kwa kusepa na pointi tatu mazima msafara wa Yanga umeanza safari kuelekea Mali.

Februari 22 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma KMC 0-1 Yanga na kuipa pointi tatu Yanga ikiwa inaongoza ligi.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Clemnt Mzize akiwa ndani ya 18 akitumia makosa ya kipa wa KMC David Kissu kwenye harakati za kuokoa kona.

Leo Yanga imeanza safari kuelekea Mali kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako unaotarajiwa kuchezwa Februari 26,2023.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye msafara huo ni Tuisila Kisinda, Farid Mussa, Aziz KI, Fiston Mayele.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA
Next articleJONAS MKUDE AMPA JEURI KOCHA SIMBA