YANGA KUONGEZA HALI YA KUJIAMINI KWA KMC

KOCHA Mkuu wa KMC, Hitimana Thiery amesema kuwa watapambana kupata matokeo mazuri dhidi ya Yanga ili kurejesha hali ya kujiamini kwa wachezaji wake.

Timu hiyo ilitoka kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Ruvu Shooting kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mchezo huo waliokuwa ugenini KMC ilikwama kufurukuta mbele ya Ruvu Shooting wazee wa mpapaso.

 Thiery amesema kuwa mechi ambazo walicheza walifanya makosa ambayo yaliwafanya wakose ushindi hivyo wanafanya kazi kwenye mechi zinazofuata.

“Tulikosa matokeo kwenye mchezo uliopita na tukwenda kukutana na Yanga ambao wamekuwa kwenye matokeo mazuri tunawaheshimu na tutapambana kupata matokeo chanya.

“Hali ya wachezaji ipo vizuri na matokeo mazuri mbele ya Yanga yataupa nguvu ya kujiamini na ukiitazama ligi ushindani ni mkubwa nasi tunazidi kujiimarisha kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” amesema Hitimana.