DAKIKA 45 zimekamilika na ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma KMC 0-1 Yanga ikiwa ni mchezo wa ligi.
Kazi kubwa imefanyika kwa timu zote kusaka ushindi ambapo ni Yanga walikuwa wa kwanza kuwatungua KMC.
Bao la uongozi limejazwa kimiani na Clement Mzize ambaye alimalizia pigo la kona lililomshinda mlinda mlango David Kissu.