KIUNGO Sadio Kanoute ni lazima abadili uchezaji wake kwenye kutimiza majukumu yake anaigharimu timu, anagharimu afya za wachezaji wake.
Ni mchezaji mzuri anafanya kazi ngumu na inayoonekana lakini lazima aongeze umakini kwenye kutimiza majukumu yake.
Kuna mikato yake mingine ni hatari kwa usalama wa wachezaji na kadi za njano ambazo anapewa zinaigharimu timu yake.
Benchi la ufundi na wachezaji wenzake ni lazima wamuambie mwana kwamba mikato sawa pale panapohitajika lakini usalama wa mchezaji ni muhimu.
Dakika zake 90 mbele ya Azam FC alivuja jasho kutumiza majukumu yake na alionyeshwa kadi ya njano kutokana na mikato yake.
Isingekuwa ni nyota wa Azam FC kuwa kwenye mtego wa kuotea mambo yangekuwa ni tofauti kwani kadi nyekundu ilikuwa inamuhusu.
Ikumbukwe kwamba alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Raja Casablanca kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano na kwa namna kikosi cha Simba kilivyo kila mchezaji ni muhimu.