Home Sports YANGA 3-1 TP MAZEMBE… WANANCHI WAKIAMUA HAWASHINDWI, NGOMA ILIPIGWA NAMNA HII

YANGA 3-1 TP MAZEMBE… WANANCHI WAKIAMUA HAWASHINDWI, NGOMA ILIPIGWA NAMNA HII

WEKA ngoma ngumu Wananchi wanaicheza bila hofu kwa kuwa wapo nyumbani na burudani unapata bila tabu kwani Wananchi wakiamua hawashindwa. Ilikuwa hivyo dhidi ya TP Mazembe juzi Jumapili.

Mpanga mipango alikuwa ni Kocha Nasreddine Nabi aliyeshuhudia dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 3-1 TP Mazembe ukiwa ni mchezo wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo ngoma ilipigwa namna hii.

DJIGUI DIARRA

Kipa wa Yanga, alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 20, aliokoa hatari dakika ya 5, 15, 19, 21, 45, 45, 55, 59, 73, 74 na 90. Alipiga pasi ndefu dakika ya 7, 13, 16, 16, 22, 42, 42, 45, 51, 56, 60, 65, 81 na 83, alipiga pasi fupi dakika ya 9, 13, 42, 47 na 48.

DJUMA SHABAN

Beki wa kulia wa Yanga, alianza kupeleka balaa kwa TP Mazembe na faulo yake ya dakika ya 6 ilileta bao, pia alipiga faulo dakika ya 69, kona ilikuwa dakika ya 35 na 40, alirusha dakika ya 5 na 7, aliokoa hatari dakika ya 54.

JOYCE LOMALISA

Aliokoa hatari dakika ya 38 na 43, alirusha mpira dakika ya 25, 36 na 42. Huyu ni beki wa kushoto wa Yanga.

KENNEDY MUSONDA

Alianza kuifungia Yanga bao dakika ya 6, alitoa pasi ya bao dakika ya 10 kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18.

Dakika ya 36 na 49 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango na dakika ya 12 alipiga krosi, huku akitumia dakika 53 uwanjani, nafasi yake aliingia Aziz Ki ambaye aliokoa hatari dakika ya 62, alipiga krosi dakika ya 68, huku akipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 83.

JESUS MOLOKO

Jesus Moloko ndiye alichezewa faulo dakika ya 6, ikapigwa na Djuma Shaban na kuzaa bao la kwanza, pia alichezewa faulo dakika ya 26 na 65, aliokoa hatari dakika ya 29, akayeyusha dakika 87, nafasi yake ilichukuliwa na Clement Mzize.

DICKSON JOB

Mtu wa kazi ngumu, alikuwa ametulia kwenye eneo la ulinzi la Yanga, aliokoa hatari dakika ya 9, 23, 51 na 71, alipiga faulo dakika ya 32.

MUDATHIR YAHYA

Utulivu wake dakika ya 10 uliwanyanyua Yanga kwa mara nyingine alipofunga bao kwa mguu wa kulia akitumia pasi ya Musonda.

Alitumia dakika 66 uwanjani, aliotea dakika ya 12 na 58, nafasi yake ilichukuliwa na Tuisila Kisinda aliyepachika bao la tatu dakika ya 90.

FISTON MAYELE

Mzee wa kutetema, alikuwa kwenye harakati zake akitoa pasi ya bao dakika ya 90 kwa Kisinda akitumia mguu wa kulia akiwa nje ya 18. Dakika ya 9 alipiga shuti ambalo halikulenga lango na alicheza faulo dakika ya 88.

BAKARI MWAMNYETO

Beki na nahodha wa Yanga, aliokoa hatari dakika ya 12, 23, 29, 47, 47, 61, 67 na 90 alicheza faulo dakika ya 14 ambapo alionyeshwa kadi ya njano, nyingine ilikuwa dakika ya 79.

KHALID AUCHO

Alicheza faulo dakika ya 27 na 44, aliokoa dakika ya 82, alikuwa akicheza eneo la kiungo la Yanga.

YANNICK BANGALA

Alitumia dakika 87 uwanjani, aliokoa hatari dakika ya 15, 17, 47 na 85, akalifanya lango la Yanga kuwa salama, nafasi yake ilichukuliwa na Zawad Mauya.

NARCISSE NLEND

Kipa huyu wa TP Mazembe, alitunguliwa mabao matatu, alifanikiwa kuoko hatari dakika ya 40, 51, 62, 69 na 77.

CHRISTINA KOUAME

Nahodha wa TP Mazembe, aliokoa hatari dakika ya 32, alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 5.

PHILIPPE KINZUMBI

Ni dakika ya 28 na 70, alipewa majukumu ya kupiga faulo dakika ya 5 alicheza faulo huku akipiga mashuti yaliyolenga lango dakika ya 21 na 45.

ALEX GONGA

Aliwapa tabu Yanga, lakini walifanikiwa kumdhibiti licha ya kuwatungua bao moja dakika ya 80 kwa pigo la faulo akiwa nje kidogo ya 18. Ni dakika ya 8 alipiga shuti ambalo lililenga lango huku akichezewa faulo dakika ya 14 na 24.

KELVIN MONDEKA

Aliokoa hatari dakika ya 32, 39, 49, 63 na 71, alipewa kazi ya kurusha dakika ya 57.

ADAM BOSSU

Mwamba huyu alipiga mashuti dakika ya 28 na 49 ambayo hayakulenga lango, ilikuwa dakika ya 27 na 78 alichezewa faulo.

GLODY LIKONZA

Alianza eneo la kiungo, alitolewa dakika ya 34, aliingia Mukoko Tonombe ambaye alichezewa faulo dakika ya 43, 44 na 69, alicheza faulo dakika ya 49 na 64, alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 59 na 83.

TANDI MWAPE

Kazi kubwa alifanya ikiwa ni dakika ya 49 na 66 alipopiga krosi, faulo yake ya dakika ya 68 ilimpa zawadi ya kadi ya njano.

Previous articleYANGA SC YAMTEKA WINGA TP MAZEMBE,NABI AFICHUA SIRI KIPIGO TP MAZEMBE
Next articleRASHFORD, OSIMHEN, MBAPPE HAWAZUILIKI