SIMBA 0-1 AZAM FC

NI bao la mapema zaidi ndani ya Ligi Kuu Bara kupata kutunguliwa kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula na mtupiaji akiwa ni mshikaji wake anayempa mateso siku zote.

Anaitwa Prince Dube hakuhitaji dakika mbili zaidi ya ile ya kwanza kupachika bao la uongozi dhidi ya Simba kwenye mchezo unaochezwa Uwanja wa Mkapa.

Moja ya mchezo ambao umekusanya kadi nyingi za njano ambapo mchezaji wa kwanza kuonyeshwa ni
Kennedy Juma wa Simba hata mfungaji Dube naye ana kadi ya njano.

Simba nafasi zake ambazo imetengeneza za hatari ni mbili pekee huku wakikosa umakini eneo la umaliziaji ndani ya dakika 45 za mwanzo.