AZAM FC HAINA PRESHA NA SIMBA

KALI Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa maandalizi ambayo wanafanya kwa sasa ni kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba.

Azam FC inatarajiwa kumenyana na Simba, Februari 21 Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi.

Ongala amesema kuwa wachezaji hawana hofu na mechi kubwa zaidi ya kuwa na hamasa na utayari wa kupata matokeo.

“Kwenye mechi kubwa hakuna presha kwa sababu wote ambao tunakutana nao tunatambuana vema na ukiangalia aina ya wapinzani wetu na sisi wote tunahitaji matokeo.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini kupata matokeo ni kitu muhimu, tupo tayari na maandalizi yapo vizuri,” alisema.

Mechi mbili za kirafiki Azam FC imecheza dhidi ya KMKM na Mlandege ambapo zote imeshinda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba.