KIUNGO Aziz KI mali ya Yanga huenda asianze kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa kesho kutokana na kutokuwa fiti.
Yanga kesho ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe.
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho na wamefanyia kazi makosa kwenye mchezo uliopita.
“Makosa kwenye mchezo wetu uliopita tumefanyia kazi na sasa ni kwa ajili ya maandalizi ya mwisho na tuna amini kwamba tutafanya vizuri.
“Azizi KI hakuwa na timu kwenye mazoezi kwa muda wa siku mbili kutokana na matatizo ya kifamilia hivyo tutaangalia kuhusu kuanza kwake.
“Pia Sure Boy naye ana matatizo ya kifamilia hivyo hatakuwa kwenye kikosi wengine wote wapo tayari,”.