BALAA zito kwenye benchi la ufundi la Simba wakitoka kuyeyusha pointi tatu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika watakosa huduma ya kiungo wao mgumu Sadio Kanoute.
Kazi kubwa itakuwa kwa benchi la ufundi kupasua kichwa kuamua wataanza na yupi kati ya Ismail Sawadogo, Mzamiru Yassin ama Jonas Mkude ikiwa atakuwa fiti.
Kanoute alionyeshwa kadi za njano kimataifa ya kwanza ubao uliposoma Simba 2-0 Big Bullets mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa Septemba 18,2022 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 60.
Pia kwenye mchezo dhidi ya de Agosto uliochezwa Uwanja wa de Novembro Oktoba 9,2022 Simba ilishinda 1-3.
Kanoute mtembeza mabuti kimyakimya alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 79 ngoma imedunda mpaka kwenye hatua ya makundi walipokutana na Horoya ugenini.
Wakati ubao wa Uwanja wa General Lansana Conte uliposoma Horoya 1-0 Simba mwamba alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 60.
Kiungo huyo wa kazi ngumu hatakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Raja Casablanca unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 18 kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano.