DAKIKA 45 za mwanzo zimemeguka ambapo ubao unasoma US Monastir 2-0 Yanga wawakilishi kutoka Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Ni Mohamed Saghroui dakika ya 10 na Boubacar Traore ilikuwa dakika ya 15.
Djigui Diarra anatimiza majukumu yake akiwa ameokoa hatari moja iliyokuwa ni nafasi ya wazi kwa wapinzani wao kufunga ilikuwa dakika ya 12.
Jesus Moloko na Djuma Shaban wamekuwa wakibadilishana upande ili kumwaga majalo ndani ya 18 kumsaka Fiston Mayele ambaye ameanza kikosi cha kwanza.
Pia Sure Boy na Aucho wapo eneo la kati kwenye upande wa viungo kusambaza upendo wakiwa wanaongoza kwa umiliki bado kupata bao.