HAKUNA mbabe ndani ya dakika 90 baada ya kutoshana nguvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Wakati Ihefu ikigawana pointi mojamoja na Singida Big Stars kwa kufungana bao 1-1 nyota Nivere Tigere penalti yake imeokolewa na mlinda mlango Benedict Haule.
Mchezo huo umechezwa leo Februari 12 huko Mbeya,Mbarali.
Ngoma Uwanja wa Highland ilikuwa ngumu kwa timu zote zikipambana kusaka pointi tatu.
Ni Meddie Kagere dakika ya 63 alianza kupachika bao kwa Singida Big Stars ambalo liliwanyanyua mashabiki wa timu hiyo.
Ingizo jipya Yacouba Songne ndani a Ihefu akitokea benchi alipachika bao la kuweka usawa dakika ya 77 kwenye mchezo huo.
Ihefu inafikisha pointi 27 ikiwa nafasi ya 8 na Singida Big Stars inafikisha pointi 44 ikiwa nafasi ya tatu.