WAKIWA ugenini nchini Tunisia wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika wamepoteza mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi.
Dakika 90 ubao wa Uwanja wa Olympic Rades umesoma US Monastir 2-0 Yanga.
Pointi tatu zimeyeyuka mazima ugenini kwa Yanga ambayo ilifanikiwa kwenye umiliki wa mpira muda wote huku wapinzani wao wakimaliza kazi ndani ya dakika 30.
Mabao ya US Monastir yalipachikwa dakika ya 10 mtupiaji akiwa ni Mohamed Saghroui na dakika ya 15 na mtupiaji akiwa ni Traore.
Mshambuliaji Fiston Mayele wa Yanga jitihada zake kusaka bao akishirikiana na wachezaji wengine ikiwa ni pamoja na Aziz KI, Sure Boy, Yannick Bangala ziligonga mwamba.