NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua uimara wa wapinzani wao US Monasti hivyo wanajipanga kusaka ushindi.
Kesho Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ukiwa ni mchezo wa kwanza kwenye makundi.
Nabi ameweka wazi kuwa anawatambua wapinzani wao ni moja ya timu imara na inaushindani mkubwa jambo watakalofanyia kazi.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya US Monastir na ninawatambua wapinzani wetu kuwa ni timu imara.
“Timu hiyo inatoka eneo ambalo nimezaliwa hivyo ni moja ya timu imara na yenye ushindani mkubwa,”
Miongoni mwa wachezaji ambao wamefanya mazoezi ya mwisho leo ni pamoja na Zawad Mauya, Dickson Job, Fiston Mayele na Jesus Moloko.