SAMBALOKETO anga za kimataifa kwa Simba limekwama baada ya kuhushudia wakiyeyusha pointi tatu ugenini.
Dakika 90 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ubao umesoma Horoya 1-0 Simba.
Bao la ushindi kwa Horoya limepachikwa dakika ya 18 na Pape Ndiaye aliyetumia makosa ya mabeki kushindwa kwenda naye sawa wakati wa pigo la kona.
Akiwa huru aliruka juu na kuachia kichwa kilichomshinda Air Manula ambaye aliokoa penalti moja kwenye mchezo huo.