SIMBA NDANI YA GUINEA

MSAFARA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira umewasili Guinea kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 12 siku ya Jumamosi ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kundi C kwa timu hizo.

Msako wa pointi tatu kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kutoka Tanzania utaanzia ugenini.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara ni pamoja na Moses Phiri, Sadio Kanoute, Pape Sakho, Mzamiru Yassin na Shomary Kapombe.

Kwa upande wa viongozi ni pamoja na Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula.

Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa.