>

MESSI NA CR 7 BALAA LAO BAADA YA MIAKA 30

WOTE wawili Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamefanya mambo ya kihistoria kwenye soka kiasi kwamba wanaonekana ni wachezaji bora wa miaka yote duniani.

Alipoingia katika muongo wake wa nne Juni 2017, Messi alikuwa moto na kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Barcelona na ametumia miaka yake 30 kudhihirisha kuwa yeye ndiye mwanasoka bora zaidi wa wakati wote.

Lakini miaka yake ya mwisho akiwa Barcelona iliambatana na kuzorota kwa uchumi klabuni hapo. Baada ya kuaga huku akitokwa na machozi, Messi alijiunga na PSG akiwa na umri wa miaka 34.

Muargentina huyo alianza kwa shida katika msimu wake wa kwanza pale Paris, Ufaransa, lakini bado alishinda taji la Ligue 1. Amekuwa bora zaidi katika msimu wa pili, huku katikati ya miaka 30 akiiongoza timu ya Taifa ya Argentina kutwaa Copa America na Kombe la Dunia la Klabu.

Wakati huohuo, Ronaldo alifikisha miaka 30 Februari 2015 akiwa na Real Madrid na baadaye kidogo akabeba mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Baada ya hapo, mwaka 2018 akahamia Juventus na kutoweka kiasi kisha akarejea Manchester United. Ronaldo ametumia kipindi cha pili cha maisha yake ya uchezaji akigubikwa na sifa chafu za kibinafsi kiasi cha kuvunjiwa mkataba wake Old Trafford.

Kwa sasa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa kimataifa akiwa tayari ana mataji ya Euro na UEFA Nations League aliyotwaa akiwa na timu ya Taifa ya Ureno – wote Ronaldo na Messi tayari wameshatwaa Tuzo ya Ballon d’Or.

Lakini wawili hawa unawapambanisha vipi kwa takwimu zao baada ya miaka 30 kwenye maisha yao kisoka? Jibu liko hapa.

CRISTIANO RONALDO

Mechi: 429

Mabao: 357

Asisti: 79

Penalti (Asilimia): 72 (79.1%)

Bao kwa dakika: 102.1

Dakika bila bao la penalti: 127.8

Bao/asisti kwa dakika: 83.2

MATAJI

– 1 x La Liga (2016-17)

– 1 x Supercopa de Espana (2017)

– 3 x UEFA Champions League (2015-16, 2016-17, 2017-18)

– 2 x Kombe la Dunia la Klabu (2016, 2017)

– 2 x UEFA Super Cup (2016, 2017)

– 2 x Serie A (2018-19, 2019-20)

– 1 x Coppa Italia (2020-21)

– 2 x Supercoppa Italiana (2018, 2019)

– 1 x European Championship (2016)

– 1 x UEFA Nations League (2018-19)

TUZO BINAFSI

– 2 x Ballon d’Or (2016, 2017)

– 2 x Mchezaji Bora wa Kiume wa Fifa (2016, 2017)

– 1 x Mfungaji Bora Ulaya (2014-15)

– 1 x Mfungaji Bora Euro (2016)

– 2 x Mchezaji Bora wa Mwaka wa Serie A (2018-19, 2019-20)

– 1 x Pichichi Trophy (mfungaji bora La Liga)

– 1 x Capocannoniere (Mfungaji bora Serie A) (2020-21)

– 1 x Tuzo Bora Maalum ya FIFA kwa Mafanikio Bora ya Kazi (2021)

LIONEL MESSI:

Mechi: 306

Mabao: 230

Asisti: 118

Penalti (asilimia): 34 (75.5%)

Bao kwa dakika: 113.3

Dakika bila bao la penalti: 133.0

Bao/asisti kwa dakika: 74.9

MATAJI ALIYOSHINDA

– 2 x La Liga (2017-18, 2018-19)

– 2 x Copa del Rey (2017-18, 2020-21)

– 1 x Supercopa de Espana (2018)

– 1 x Ligue 1 (2021-22)

– 1 x Trophee des Champions (2022)

– 1 x Copa America (2021)

– 1 x Artemio Franchi Cup (2022)

– 1 x Kombe la Dunia (2022)

TUZO BINAFSI

– 2 x Ballon d’Or (2019, 2021)

– 1 x Mchezaji Bora wa Kiume wa Fifa (2019)

– 2 x Mfungaji Bora Ulaya (2017-18, 2018-19)

– 1 x Mchezaji bora Kombe la Dunia (2022)

– 1 x Mchezaji Bora Copa America (2021)

– 4 x Pichichi Trophy (Mfungaji bora La Liga) (2017-18, 2018-19, 2019-20, 2020-21)