AZAM FC YAANZA MATIZI KUMVUTIA KASI MNYAMA

KIKOSI cha Azam FC kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo imetoka kupoteza mchezo wake uliopita kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma ukisoma Dodoma Jiji 2-1 Azam FC.

Februari 21,2023 saa 1:00 usiku Azam FC itakuwa kwenye kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Simba.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Prince Dube aliyepeleka kilio Msimbazi.

Ni Februari 8 kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala kilianza mazoezi Uwanja wa Azam Complex.

Miongoni mwa wachezaji ambao wameanza mazoezi ni pamoja na Dube, Tepsi Evance, Idd Suleiman, ‘Nado”.