MZAWA JOB AWEKA REKODI TAMU BONGO

MZAWA Dickosn Job anayekipiga ndani ya kikosi cha Yanga ameweka rekodi yake matata kwa kuwa mzawa pekee ambaye amefunga kwa timu za Kariakoo Februari ndani ya Uwanja wa Mkapa.

Mechi za ufunguzi wa Februari, Simba na Yanga zote zimecheza Uwanja wa Mkapa na kusepa na ushindi ilianza Simba Februari 3 ubao uliposoma Simba 3-1 Singida Big Stars.

Kwenye mchezo huo mabao ya Simba yote yalifungwa na wageni ilikuwa ni Jean Baleke wa Dr Congo, Saidi Ntibanzokiza wa Burundi hawa walitumia pasi za Clatous Chama wa Zambia na Pape Sakho kutoka Senegal aliyetumia pasi ya beki mzawa Shomary Kapombe.

Hata bao la Singida Big Stars lilipachikwa na Bruno Gomez ambaye ni raia wa Brazil hivyo kwenye mabao manne yaliyofungwa hakuna mzawa aliyefunga zaidi ya pasi moja ya Kapombe.

Job alivunja mwiko huo kwa kupachika bao moja Februari 4 ubao uliposoma Yanga 2-0 Namungo FC akitumia pasi ya Djuma Shaban ambaye alipiga kona Uwanja wa Mkapa na bao la pili lilifungwa na Aziz KI.

Kwenye mabao sita ambayo yamefungwa Uwanja wa Mkapa, mzawa mmoja tu kafunga ambaye ni Job na kwa pasi pia ni mzawa mmoja katoa ambaye ni Kapombe wa Simba ndani ya ligi.