Home Sports AKILI KUBWA MZUNGUKO WA PILI MATUMIZI YA NGUVU NI MAUMIVU

AKILI KUBWA MZUNGUKO WA PILI MATUMIZI YA NGUVU NI MAUMIVU

MZUNGUKO wa pili huwa unakuwa na mambo mengi jambo ambalo huwafanya wachezaji wengi kutumia nguvu kubwa kusaka ushindi.

Ukweli ni kwamba mechi za wakati huu ni lala salama kwa kuwa kitakachofuata ni maamuzi ya nini kitatokea kwa kile ambacho kimepandwa.

Benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki muda wa kujipanga kwa makosa ya mzunguko uliopita ni sasa na itasaidia kuwa kwenye ushindani mzuri.

Mashabiki na benchi la ufundi bila kusahau wachezaji wanapokuwa uwanjani hesabu zao ni kuona kwamba wanashinda hivyo wakikosa ushindi huzuni huwa inakuwa juu yao.

Haina maana kwamba mashabiki hawajui kuhusu ushindani uliopo wanajua lakini ni muhimu kuwepo na furaha pia sio kila wakati huzuni.

Wengi wanaamini wakitumia nguvu kubwa watapata matokeo makubwa na kusahau kwamba kinachotafutwa ni pointi tatu na sio matumizi ya nguvu.

Kwa wakati huu ambao upo ni muhimu kila timu kufanya maandalizi ili iweze kupata kile ambacho inastahili. Mashabiki wanahitaji ushindi na wapinzani wao pia wanahitaji ushindi nadhani unapata picha ushindani ulivyo.

Huu ni mzunguko ambao unakuwa na maamuzi ya nani atakuwa nani na wapi kwa sababu gani. Ikiwa hakuwatakuwa na mipango makini basi wakayi wenyewe utapanga mipangilio na matokeo yataonekana uwanjani.

Kikubwa ni utulivu na matumizi mazuri ya nguvu kila mchezaji awe ni mlinzi wa mchezaji mwenzake ili kumpa nafasi ya kucheza kwa kujiamini kufikia malengo yake.

Previous articleLIGI KUU TANZANIA BARA KUKIWASHA LEO
Next articleMAYELE ANATOA SOMO LA BURE KWA WENGINE