BADO KAZI INAENDELEA, HAKUNA KUKATA TAMAA

MIGUSO ya furaha inaonekana kuanza kuyeyuka kwa baadhi ya mashabiki kutokana na timu zao kushindwa kupata matokeo kwenye mechi za Kombe la Shiriksho.

Hakika kila mmoja anapenda kuona kile anachofikiria kinafanikiwa na ikiwa ngumu kutokea inakuwa ngumu kuamini.

Imeshakuwa hivyo hakuna namna nyingine ya kuzuia kwa sababu mpira ni mchezo wa makosa yule ambaye atakosea mara moja safari yake ya maumivu inakuwa inamuhusu.

Haina maana kwamba wao hawawezi hapana, haina maana kwamba vipaji kwao havipo hapana bali ni matokeo na kilichotokea huwezi kukibadili kwa sasa mpaka wakati ujao.

Pongezi kwa wale ambao wamepata ushindi kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, tumeona ushindani wa kweli na hili linastahili kila wakati.

Kuna timu ambaz zinacheza kwa umakini mpaka unajiuliza ni walewale ama wengine, basi juhudi ambazo zilikuwa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho na zihamie ndani ya ligi.

Wachezaji wameonyesha ukomavu kwa kucheza kwa nidhamu kubwa kwenye hatua hii na hapo inaonyesha kwamba kila kitu kinawezekana.

Wale ambao safari imegota mwisho haina maana kwamba hakuna maisha mengine bado kuna mashindano mengine yanakuja na huku ni muhimu kujipanga.

Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi ni lazima maisha ya mpira yaendeleee na kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati.