MIKATO yake anayotembeza kimyakimya ndani ya uwanja leo Sadio Kanoute kaihamishia kwa mlinda mlango wa Coastal Union.
Ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 1-0 Coastal Union dakika ya 56 akiwa nje ya 18 na kuwanyanyua mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo.
Coastal Union walicheza kwa kujilinda muda mwingi jambo lililowapa ugumu Simba iliyomtumia Jean Baleke kupata tabu kushinda kwenye mchezo huo.
Kwenye mchezo huo Manzoki alikuwa shuhuda namna Simba ilivyokuwa inapata tabu kupenya mbele ya Coastal Union.