SINGIDA BS YAISHTUKIA YANGA KWA GOMES

MABOSI wa Singida Big Stars kwa sasa jicho lao ni kwa wachezaji wao wote wanaofanya vizuri ili wawaongezee dili jipya na miongoni mwa nyota anayetazamwa kwa ukaribu ni Bruno Gomez.

Gomez raia wa Brazil ni mtambo wa mabao akiwa nayo nane huku akizitungua timu 7, anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa mitaa ya Kariakoo, Simba na Yanga.

Habari zinaeleza kuwa mabosi wa timu hizo kwa sasa wanaendelea kutazama wachezaji wanaofanya vizuri kunasa saini zao na jina la Gomes linajadiliwa.

Taarifa kutoka Singida Big Stars zimeeleza kuwa kwa sasa hakuna mchezaji ambaye atasepa ndani ya kikosi hicho ikiwa watakuwa wanamhitaji kutokana na umuhimu wake.

Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Massanza ameweka wazi kuwa kwa mwendo anaokwenda nao Gomez kuna umuhimu wa kumuongezea mkataba.

“Kuna umuhimu wa kumuongezea mkataba wetu kiungo Gomez kutokana na uwezo wake hivyo kwa wale ambao wanafikiria kumpata kazi ipo,” alisema.

Nyota huyo rekodi zinaonyesha kwamba akifunga bao kwenye mchezo wa ligi basi wapinzani hawaambulii pointi tatu ndani ya dakika 90.