ENEO ambalo KMC wanapaswa kuboresha na kuongeza nguvu kwa mzunguko huu wa pili ni ulinzi ikiwa ni beki na mlinda mlango.
Kipa wao namba moja David Kissu amekuwa akifanya makosa mengi yakizembe akiwa langoni hasa kutokana na maamuzi yake yanayoigharimu timu.
Alipata tabu akiwa langoni kutokana na kutunguliwa mabao akiwa langoni.
Anaingia kwenye orodha ya makipa waliotunguliwa hat trick ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.
Ilikuwa ni Januari 24,2023 Uwanja wa Uhuru ubao uliposoma KMC 1-3 Namungo FC ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili.
Mabao yote ya Namungo yalipachikwa kimiani na Ibrahim Mkoko ilikuwa dakika ya 40,57 na 90 huku lile la KMC likipachikwa kimiani na Kelvin Kijili dakika ya 59.
Kwenye mchezo mwingine ambao ulichezwa Januari 24,2023 Geita Gold 1-0 Coastal Union ambapo bao lilipachikwa na Edmund John dakika ya 59.