BRUNO AWATULIZA MATAJIRI WA DAR

REJEA andiko kwenye makala ya gazeti la Championi Jumamosi la Januari 21,2023 ukurasa wa tano.

Labda ulikuwa na mambo mengi umesahau ngoja nikukumbushe kichwa cha habari cha makala hiyo, ‘Bruno Gomez… Akikufunga, pointi tatu sahau…

Wakati makala inaandikwa tayari mwamba alikuwa ametupia kambani mabao 7 kwenye mechi sita na zote Singida Big Stars walisepa na pointi tatu mazima.

Kabla Januari haijameguka,Azam FC wamekutana na jambo leo Januari 23, Uwanja wa Singida Big Stars.

Ni yeye Gomez ambaye alitupia bao dakika ya 45 kw pigo la faulo nje kidogo ya 18, bao moja la maajabu kwa kuwa hakuna aliyetarajia kwamba angefunga na hakupiga hatua nyingi kukamilisha pigo hilo.

Azam FC imeyeyusha pointi tatu ikiwa Uwanja wa Liti kwa kutunguliwa bao moja lililoamua matokeo kwenye mchezo wa leo.