KIBINDONI ana mabao 7 ndani ya Ligi Kuu Bara nyota huyu wa Singida Big Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Hans Pluijm.
Bao lake la saba aliwatungua Kagera Sugar ilikuwa Uwanja wa Liti, Januari 17 ubao uliposoma Singida Big Stars 1-0 Kagera Sugar ilikuwa dakika ya nne.
Baada ya kutupia bao hilo alionyesha fulana yenye maneno ambayo sio lugha ya Bongo kwa tafsri isiyo rasmi ilikuwa inasema:”Pumzika kwa Amani. Nitakupenda milele ndugu yangu Samuel”
Huo ulikuwa ni ujumbe maalum kwa rafiki yake aliyefariki siku chache zilizopita huko nchini Brazil.
Kituo kinachofuata kwa timu hiyo ni dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Liti Jumatatu.