RIPOTI KUAMUA HATMA YA TAMBWE, KAGERE, SINGIDA BIG STARS

UONGOZI wa Singida Big Stars umeweka wazi kuwa hatma ya nyota wao ambao hawajashiriki Kombe la Mapinduzi itajulikana hivi karibuni baada ya ripoti kukamilika

Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza amesema kuwa wachezaji hao  hawakuhsiriki kombe hilo kwa sababu maalumu.

“Tambwe ni mchezaji wetu na amecheza zaidi ya mechi 12 za ligi na amekosekana katika Kombe la Mapinduzi kutokana na ruhusa maalumu ya sikukuu.

“Wapo wachezaji wengi ambao wamepewa mapumziko na ruhusa maalumu ya sikukuu ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere,Wawa, Andambwile na baadhi yao wapo ambao watatolewa kwa mikopo.

“Ripoti kamili itatolewa hivi karibuni kuhusu wachezaji wetu hivyo subira inahitajika katika hilo,”.

Kwenye mchezo dhidi ya Kager Sugar, Uwanja wa Liti Januari 17 wakati ubao ukisoma Singida Big Stars 1-0 Kagera Sugar, Kagere alianzia benchi.