MASHABIKI wa Simba leo Januari 18,2023 wanatarajia kuona ujuzi wa Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ambaye anashikirikiana na mzawa Juma Mgunda..
Mchezo wa leo ni dhidi ya Mbeya City inayotumia Uwanja wa Sokoine kwenye mechi za nyumbani.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Katika mchezo huo Simba walianza kupachika bao kupitia kwa Mzamiru Yassin na Mbeya City wakapata bao kupitia kwa Tariq Seif.