“TUMEREJEA kutoka kambi ambayo imekuwa na manufaa makubwa na kazi inaendelea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika,” maneno ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally.
Leo Januari 17,2023 kikosi hicho kimerejea kutoka Dubai ambapo kiliweka kambi kwa muda chini ya Kocha Mkuu, Robert Oliviera na msaidizi Juma Mwambusi.
Kwenye kambi hiyo maalumu ambayo imegharamiwa na Rais wa heshima ndan ya Simba, Mohamed Dewji, ‘Mo’ walicheza mechi mbili za kirafiki, walinyooshwa mchezo mmoja na kuambulia sare ya kufungana mabao 2-2.
Ni Habib Kyombo ambaye ni mzawa alipata nafasi ya kufunga kwenye mechi ya pili mabao yote mawili.
Kwa sasa timu hiyo inakwenda kufanya maandalizi ya mwisho dhidi ya Mbeya City mchezo unaotarajiwa kuchezwa kesho Januari 18,2023 Uwanja wa Mkapa.
Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye msafara huo ni Joash Onyango, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na nahodha John Bocco.