USIKU WA KISASI, YANGA 0-0 IHEFU

DAKIKA 45 za mwanzo zimekamilika ambapo ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 0-0 Ihefu.

Mbinu za Ihefu FC kwenye dakika 45 zakujilinda zimefanikiwa huku kwenye upande wa ushambuliaji wakiwa na tatizo.

Dakika 45 rekodi zinaonyesha kwamba hakuna shuti ambalo limelenga lango licha ya Obrey Chirwa na Adam Adam kuwa kwenye eneo la ushambuliaji.

Yanga wao kasi yao kwenye usiku wa kisasi ni kubwa ambapo wanafanya majaribio kupitia kwa Tuisila Kisinda ambaye amekosa utulivu katika kutumia mipira anayotengewa na Djuma Shaban.

Dakika 45 za kipindi cha pili mazungumzo ya benchi la ufundi yataamua namna gani ubao utasoma.

Moja ya mchezo ambao umetawala na ujuzi mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na uzoefu wa wachezaji wa timu hizo.