YANGA YAIVUTIA KASI IHEFU

BAADA ya kuenguliwa kwenye Kombe la Mapinduzi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufugana dhidi ya Singida Big Stars kikosi cha Yanga kimeanza maandalizi kuikabili Ihefu.

Mchezo huo ni wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumatatu ya wiki ijayo.

Ihefu ambayo mchezo wa mzunguko wa kwanza iliwatungua Yanga mabao 2-1 itakabiliana nao Januari 16,2023.

Leo ni Januari 12 ikiwa ni kumbukizi ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kesho Januari 13,2023 inatarajiwa kuchezwa fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Ni Singida Big Stars ambao walikusanya pointi nne kwenye hatua ya makundi na kutinga hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 4-1 Azam FC itakuwa dhidi ya Mlandege.

Kwenye Kombe la Mapinduzi mshambuliaji Yacouba Songne alitumika kwa kuwa alikuwa kwenye majaribio ili benchi la ufundi lione kama yupo fiti kurejea kikosi cha kwanza.

Heri ya Mapinduzi Day.