SINGIDA BIG STARS WANAIFIKIRIA FAINALI

SINGIDA Big Stars hesabu zao kwa sasa ni fainali ya Kombe la Mapinduzi, Januari 13,2023 dhidi ya Mlandege.

Timu hiyo inayonlewa na Kocha Mkuu, Hans Pluijm imetinga hatua hiyo kwa kuichapa mabao 4-1 Azam FC.

Mtupiaji wa mabao yote ya Singida Big Stars ni Francy Kazadi ambaye kibindoni anafikisha mabao matano na lile la Azam FC lilifungwa na Sopu.

Mlandege hawa waliwatungua Simba kwenye hatua ya makundi na kuwavua ubingwa mazima na walitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penalti 5-4 Namungo baada ya sare ya kufungana bao 1-1 kwenye muda wa kawaida.

Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu lakini wapo tayari.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu na tunajua itakuwa fainali ngumu ila tupo tayari na tunahitaji ushindi,”