LILE BEKI LA KAZI YANGA HILI HAPA

YANGA ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la beki wa kati kutoka Mali ili kujiunga na timu hiyo kwenye dirisha hili dogo.

Ni beki wa kati raia wa Mali Mamhadou Doumbia umri wake ni miaka 27.

Doumbia moja kati ya mabeki bora ambao wamekuwa wakiitwa katika kikosi cha Mali kinachoshiriki mashindano ya CHAN akiwa na klabu ya Stade Malien.

Doumbia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Mali inayoshiriki Mashindano ya CHAN inayowahusu wachezaji wa ndani.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ameweka wazi kuwa wanamshusha beki wa kazi ambaye anapenda kutumia mapigo ya kona kufunga,

“Tunamshusha beki wa kazi ambaye anapenda mapigo ya kona kuliko penalti, wapinzani wetu wajiandae,”.