SIMBA YASHUSHA STRAIKA WA KAZI

ZIKIWA zimebaki siku saba tu kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili Januari 15, 2023, uongozi wa Simba umewashusha presha mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia watulie kwani mabosi wa timu hiyo wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kuboresha kikosi chao kwa kushusha straika mpya.

Kwenye dirisha hili dogo mpaka sasa, Simba ambao jana Jumamosi walienda Dubai kwa ajili ya kambi ya wiki moja, wamefanikiwa kumtambulisha, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ambaye amesajiliwa kutoka Geita Gold.

Saido katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara akiwa na jezi ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons, alihusika katika mabao manne, akifunga matatu ‘hat-trick’ na kutoa asisti moja.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Kupitia dirisha hili la usajili, niwatoe hofu mashabiki wa Simba kuwa uongozi wetu upo