KUISHI ni mapenzi ya Mungu na kwa kila jambo anastahili shukrani, katika hili la 2023 tunasema asante.
Aziz KI 2022 kawatesa makipa kutokana na mapigo yake huru na mabao yanayowapa kero makipa.
Hapa kwenye mwendo wa data tunakundoshea makipa waliopata tatu kutoka kwenye miguu ya Aziz KI:-
Faroukh Shikalo
Kipa namba moja kutunguliwa na Aziz KI ni Shikalo wa Mtibwa Sugar, dakika ya 90 kwa mguu wa kushoto akiwa nje ya 18
Manula
Aishi Manula, Air Manula wa Simba alikutana na mateso ya Aziz KI dakika ya 45 kwa mguu wa kushoto akiwa nje ya 18
Ahamada
Ali Ahamada, kipa wa Azam FC dakika ya 32 alitunguliwa na kiungo huyo akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto
Shekimweri
Razak Shekimweri wa Mtibwa Sugar alitunguliwa dakika ya 26 kwa pigo la faulo lililopigwa kwa mguu wa kushoto nje ya 18.
Viwanja vyake
Ni mabao matatu kawatungua makipa Uwanja wa Mkapa na bao moja Uwanja wa Manungu
Mashoto
Mabao yote ambayo kafunga katumia mguu wa kushoto
Asisti
Katoa pasi mbili za tatu za mabao akitumia mguu wa kushoto kutoa mbili na ule wa kulia moja
Imeandikwa na Dizo Click