SIMBA V PRISONS… HAPPY NEW YEAR 2023, ASANTE 2022

HAPPY New year 2023 na asante 2022, ilikuwa ni kazi iliyofanyika kwa vitendo ndani ya Uwanja wa Mkapa, Dar, uliosoma Simba 7-1 Tanzania Prisons, juzi Ijumaa ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Hapa Spoti Xtra linakuletea baadhi ya kazi nzito zilizofanywa na wachezaji kwenye msako wa pointi tatu.

AISHI MANULA

Ilikuwa ni funga mwaka ya huzuni kwake baada ya kutunguliwa bao ambalo hakuwa na namna ya kulizuia baada ya kutema mpira, kisha akaanza safari kuufuata, akaukosa na kuwekwa kimiani.

Bao hilo dakika ya 29 lilifungwa kwa utulivu mkubwa na Jeremiah Juma akimchagulia upande wa kwenda Manula baada ya kutoka kwenye lango lake na kumfanya afunge mwaka bila clean sheet.

Angalau kipindi cha pili Manula alikuwa na utulivu na aliokoa hatari dakika ya 66 kwa shuti la Ibrahim Ibrahim.

HENOCK INONGA

Haikuwa bahati kwake kufunga mwaka kwa kuyeyusha dakika 90, aligotea dakika ya 20, alipochezewa faulo ya hatari na Samson Mbangula.

Mbangula alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi wa kati akifunga 2022 na kadi nyekundu huku timu yake ikipoteza pointi tatu.

MZAMIRU YASSIN

Kiungo wa kazi ngumu, alitoa pasi mbili za mabao dakika ya 64 na 69 akitumia mguu wa kulia. Alipiga shuti dakika ya 50 ambalo lililenga lango.

SAIDI NTIBAZONKIZA

Alitupia kambani mabao matatu ikiwa ni mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Simba baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Geita Gold.

Ilikuwa dakika ya 60, 64 na 69 ikiwa ni mashuti yaliyolenga lango na dakika ya 37, 40 na 41 alipiga mashuti yaliyolenga lango lakini yaliokolewa na kipa Hussein Abel.

Dakika ya 37 na 42 alipiga kona huku dakika ya 52 akimwaga krosi na alipiga faulo dakika ya 5 huku akikosa nafasi ya wazi kufunga dakika ya 57.

JOHN BOCCO

Nahodha John Bocco kafunga mwaka 2022 akiwa ametupia hat trik mbili ya kwanza, ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting na ya pili dhidi ya Prisons. Ilikuwa dakika ya 12, 46 na 62 anafikisha mabao 9 msimu huu wa 2022/23.

CLATOUS CHAMA

Mwamba wa Lusaka akiwa uwanjani kwa sasa yupo kila upande, alichezewa faulo dakika ya 4, alipiga faulo dakika ya 16, 43, alipiga kona dakika ya 37, 73 na 80. Alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 39 na 45, alitoa pasi moja dakika ya 60 akifikisha pasi 11 za mabao akiwa ni namba moja kwa watengeneza mipango ya mwisho 2022.

SHOMARI KAPOMBE

Beki wa Simba, alimwaga krosi dakika ya 11, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 53 na alifunga bao dakika ya 88 akimaliza krosi ya Gadiel Michael ambaye aliingia dakika ya 78 akichukua nafasi ya Mohamed Hussein.

JOASH ONYANGO

Aliokoa hatari dakika ya 12, alichezewa faulo dakika ya 20 na 76 na alicheza faulo dakika ya 17.

PAPE SAKHO

Alikuwa kwenye ubora wake na utulivu mkubwa kwenye mchezo wa funga mwaka akitoa pasi ya bao dakika ya 46 kwa Bocco na alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 37. Aliyeyusha dakika 72, nafasi yake ilichukuliwa na Augustine Okrah.

SADIO KANOUTE

Alicheza faulo dakika ya 27 na 56, akaonyeshwa kadi ya njano.

MOHAMED HUSSEIN

Maarufu kama Zimbwe Jr, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 45.

HUSSEIN ABEL

Kipa wa Prisons, alikuwa kwenye kazi kubwa katika kutimiza majukumu yake, licha ya kufungwa mabao saba, lakini aliokoa hatari dakika ya 37, 39, 41, 45 na 77. Amefunga mwaka kinyonge kwa kuwa kipa wa kwanza kutunguliwa mabao mengi mchezo mmoja.

JUMANNE ELIFADHILI

Aliokoa hatari dakika ya 4 na 73 kuelekea kwenye lango la Abel.

JOSHUA NYANTINI

Alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 4.

SALUM KIMENYA

Alipewa majukumu ya mapigo huru ikiwa ni dakika ya 34 na 51 alicheza faulo dakika ya 4, 16, 18 na 58, akiokoa hatari dakika ya 38 na 49.

NURDIN CHONA

Alikoa hatari dakika ya 5, 6, 37 kwenye mchezo huo.

SAMSON MBANGULA

Alicheza faulo dakika ya 1 na 20, zote alimchezea Inonga na alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 20.

JEREMIAH JUMA

Aliokoa hatari dakika ya 68, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 44, alimtungua Manula dakika ya 29, aliyeyusha dakika 74, nafasi yake ikachukuliwa na Edwin Balua ambaye alicheza faulo dakika ya 76.