SIMBA YATAJA SABABU YA KUTUNGULIWA NA MLANDEGE

GADIEL Michael, nahodha wa Simba kwenye kikosi kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi ameweka wazi kuwa sababu zilizofanya wakapoteza mchezo wa kwanza ni kushindwa kutumia nafasi.

Ikiwa Uwanja wa Amaan, ilishuhudia ubao ukisoma Simba 0-1 Mlandege baada ya dakika 90 kukamilika.

Ikumbukwe kwama Simba walikuwa ni mabingwa watetezi wamemaliza mwendo katika hatua hiyo wakianza kutunguliwa mchezo wao huo.

“Tulishindwa kutumia nafasi ambazo tulitengeneza ndani ya uwanja jambo ambalo limetufanya tushindwe kupata matokeo.

“Ambacho tunamshukuru Mungu ni kwamba tumemaliza mchezo salama hivyo kwa mechi ijayo tunaamini tutafanya vizuri kupata matokeo,”.

Bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Abubakar Mwadin dakika ya 75 kutokana na makosa ya ulinzi wa nyota wa Simba huku langoni akiwa alianza Beno Kakolanya.