KIUNGO WA KAZI AONGEZA MKATABA YANGA

KIUNGO wa Yanga Khalid Aucho ameongeza mkataba wa miaka miwili kusalia ndani ya kikosi hicho.

Anakuwa mchezaji wa pili kuongeza dili mpaka 2025 ndani ya Yanga.

Alianza kutangazwa Djigui Diarra kipa namba moja wa Yanga ambaye aliongeza mkataba katika kikosi hicho na kutangazwa Januari 2.

Nyota huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambapo amekuwa akifanya vizuri kwenye mechi zake.

Kwenye eneo la kati ndani ya Yanga kumekuwa na utulivu mkubwa jambo linalowapa rekodi bora ya kufanya usajili ambao umejibu.