BAO la mapema kipindi cha kwanza kwa Azam FC lililofungwa na Ayoub Lyanga halikutosha kuipa pointi tatu timu hiyo.
Ni kwenye Kombe la Mapinduzi ambalo linafanyika visiwani Zanzibar huku kila timu zikonyesha ushindani mkubwa.
Baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Azam FC 1-1 Malindi FC na kufanya matajiri hao wa Dar kugawana pointi mojamoja.
Bao la kuipa pointi moja Malindi lilipachikwa kipindi cha pili cha mchezo huo kupitia kwa Said Omary.
Nyota wa Azam FC Keneth Muguna alikabidhiwa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu kwenye mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi.
Ni mfano wa hundi wenye thamani ya laki mbili alikabidhiwa huku mchezaji bora wa mchezo akiwa ni Humoud Suleiman.