JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema maandalizi yapo sawa na wataonyesha ushindani.
“Tupo tayari kwa ushindani na tunajua kwamba haitakuwa kazi rahisi hivyo mashabiki wajue kwamba tutaonyesha ushindani.
“Wachezaji wote ambao wapo kwenye kikosi cha Simba ni mali ya Simba na wanapaswa kutumikia timu yao.
Januari 2,2023 kikosi cha Simba kiliibuka ndani ya Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Mlandege.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wapo kundi moja na KVZ, walitwaa ubingwa huo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa fainali.
Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye kikosi hicho ni pamoja na Saidi Ntibanzokiza, Kennedy Juma, Beno Kakolanya, Ally Salim, Gadiel Michael.