BRENTFORD YAANDIKA REKODI KWA KUICHAPA LIVERPOOL

KLABU ya Brentford kwenye Ligi Kuu ya Uingereza inaandika rekodi yao baada ya kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Liverpool tangu 1938 lwa ushindi wa mabao 3-1.

 Ibrahim Konate alikumbana na hali kama ile ya Wout Faes wa Leicester Ijumaa usiku, akigeuza mpira wavuni kwake bila kukusudia (19), kisha Yoane Wissa kupachika bao la pili la wenyeji akiunganisha krosi ya Mathias Jensen (42) na Bryan Mbeumo alipachika bao dakika ya 84.

 Jurgen Klopp alifanya mabadiliko mara tatu, ni Alex Oxlade-Chamberlain, alipachika bao pekee kwa Liverpool dakika ya 50.

Liverpool ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo ikiwa na pointi 28 huku Brentford ikiwa nafasi ya 7 na pointi 26.