>

WAKULIMA WAZABIBU WAFUNGA MWAKA KWA USHINDI

DODOMA Jiji waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa kufungia mwaka 2022.

Ni mabao ya Mwaterema dakika ya 24 na Opare dakika ya 66 yalitosha kuzamisha jahazi la Kagera Sugar inayotumia Uwanja wa Kaitaba kwenye mechi za nyumbani.

Ushindi huo unaifanya Dodoma Jiji kufikisha pointi 21 ikiwa nafasi ya 12 huku Kagera Sugar ikigotea na pointi zake 24 nafasi ya 6.

Pia Singida Big Stars ilisepa na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo ulioshuhudia mabao mawili yakifungwa kwa penalti.

Ni mabao ya Carno dakika ya 30 na Gomes dakika ya 80 kwa penalti ikiwa ni bao la ushindi baada ya Geita Gold kupata bao dakika ya 45 na mpigaji wa penalti kuwa ni Haruna Shamte.