>

AZIZ KI AMTUNGUA KIMWERI

UBAO wa Uwanja wa Manungu unasoma Mtibwa Sugar 0-1 Yanga.

Bao la Aziz KI dakika ya 26 linaipa uongozi timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Pigo la faulo iliyoonekana kutokuwa na hatari ilimduwaza kipa wa Mtibwa Sugar Razack Kimweri ambaye alikutana na mpira nyavuni.

Ukuta wake wa wachezaji watatu ambao aliwapanga pamoja na kutokuwa makini kwenye kuokoa pigo hilo kumewapa maumivu Mtibwa Sugar.

Pongezi kwa mpigaji namna alivyompoteza kipa ambaye hakuwa na chaguo kwenye pigo hilo lakini alifanikiwa kuokoa dakika ya 45 pigo la Aziz KI la faulo.