CEDRICK Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa walikuwa wanatambua ubora wa Azam ulipo jambo lililowafanya kuwakabili kwa mpango tofauti.
Ubao wa Uwanja wa Mkapa Desemba 25,2022 baada ya dakika 90 ulisoma Azam FC 2-3 Yanga ambapo katika mabao ya Yanga ni pasi moja ilitoka kwa kiungo mchetuaji Bernard Morrison.
Morrison alitoa pasi kwa mshikaji wake Fiston Mayele ambaye alifikisha mabao 14 ndani ya ligi akiwa ni namba moja.
“Tunajua ubora wa Azam FC hasa kwenye mapigo ya mipira ya kutengwa kama ambavyo walipata mabao kwenye mchezo ule uliopita nasi tukajipanga vizuri.
“Pongezi kwa wachezaji bado tuna kazi ya kufanya kwa mechi zetu ambazo zimebaki,” amesema.