KAZE AFICHUA WALIVYOIBANA AZAM FC KWA MKAPA

CEDRICK Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa walikuwa wanatambua ubora wa Azam ulipo jambo lililowafanya kuwakabili kwa mpango tofauti. Ubao wa Uwanja wa Mkapa Desemba 25,2022 baada ya dakika 90 ulisoma Azam FC 2-3 Yanga ambapo katika mabao ya Yanga ni pasi moja ilitoka kwa kiungo mchetuaji Bernard Morrison. Morrison alitoa pasi kwa mshikaji…

Read More

KMC 0-1 SIMBA, MAPIGANO AOKOTA MPIRA NYAVUNI

UWANJA wa CCM Kirumba dakika 45 za mwanzo zimemeguka kwa wachezaji kuvuja jasho katika msako wapointi tatu. Ubao unasoma KMC 0-1 Simba bao likifungwa na John Bocco dakika ya 15. David Mapigano kwenye mapigano ya kuokoa hatari hakuwa na chaguo la kufanya zaidi ya kuhushudia mpira ukiwa umezama nyavuni.

Read More

AZAM FC YATAJA SABABU YA KICHAPO

KALI Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa walikwama kushinda mbele ya Yanga kutokana na kushindwa kuwa makini. Azam FC jana Desemba 25 ilinyooshwa mbele ya Yanga kwenye mchezo wa ligi na kuyeyusha mazima pointi tatu. aada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 2-3 Yanga ambapo bao la ushindi lilifungwa na Farid…

Read More

MAJINA 14 YAPITISHWA NDANI YA SIMBA

KUELEKEA kwenye uchaguzi mkuu wa Simba unaotarajiwa kufanyika Januari 29,2023 kamati ya uchaguzi jana Desemba 25,2022 imetoa orodha ya wagombea 14 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali. Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Boniface Lihamwike imebainisha kuwa majina ya waliopitishwa ni wale ambao wamekidhi vigezo huku idadi ya wanaowania nafasi ya mwenyekiti ikiwa na wagombea wawili, 12 kwa…

Read More

MCHEZO MZIMA WA AZAM FC V YANGA ULIKUWA NAMNA HII

ZAWADI ya Chritmas imetolewa kwa mashabiki wa Yanga baada ya timu hiyo kutoka nyuma ilipoanza kufungwa na Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Mkapa na mwisho ukasoma Azam FC 2-3 Yanga. Ni Abdul Seleman, ‘Sopu’ alianza kumtungua kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra dakika ya 27 akitumia pasi ya Prince…

Read More

MABAO 11 YA SIMBA KUIKOSA KMC

MABAO 11 ya Simba leo yanatarajiwa kukosekana uwanjani kutokana na matatizo ya wachezaji hao. Ni Moses Phiri ambaye ni mshambuliaji namba moja akiwa ametupia mabao 10 na Peter Banda yeye ametupia bao moja. Mastaa hawa wote hawatakuwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya KMC kwa kuwa hawapo fiti jambo litakalowafanya wakosakane kwenye mchezo huo. Ikumbukwe…

Read More