RASMI mabosi wa Simba na beki wao wa kati Henock Inonga wamefikia makubaliano ya kumuongezea dili nyota huyo mpaka 2025.
Kandarasi ya Inonga ilikuwa inagota ukingoni mwishoni wa msimu wa 2022/23.
Kutokana na uwezo wake pamoja na kuwa mtu wa kazi ameongezewa dili jingine ikiwa ni zawadi ya Christmas kwa mashabiki wa Simba.
Inonga ana tuzo ya beki bora wa msimu wa 2021/22 alipokuwa ndani ya Simba.
Msimu huu kwenye ligi katupia bao moja ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.
Merry Christmas