WAAMUZI UMAKINI UNAHITAJI KWENYE MAAMUZI

UNAONA mzunguko wa kwanza ulianza kwa kelele nyingi kutokana na waamuzi kuoneana wakifanya maamuzi ambayo yalikuwa yanaleta utata kwa wachezaji pamoja na mashabiki kushindwa kuelekewa kinachoendelea.

Matukio ya kushindwa kutafsri sheria 17 yalikuwa yakiwapeleka mara kwa mara kwenye kamati za maadili kisha wakirejea wanaendelea kuwa kwenye ubor wao.

Hii inamaanisha kwamba waamuzi tulioano uwezo wanao mkubwa wa kufanya kazi na maamuzi kwa umakini lakini kuna namna ambayo inawafanya washindwe kuwa na mwendelezo mzuri.

Ilikuwa ni rahisi sehemu ambayo inapaswa kutolewa penalti kutotolewa na sehemu ambayo haikupaswa inatolewa haya ni mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa maboresho makubwa.

Tayari mzunguko wa pili umeanza huku ushindani ukizidi kuongezeka lakini sasa inaonekana na waamuzi nao wanarejea yale masuala yaliyokuwa yanapungua sasa yanaanza kurejea taratibu.

Imani yetu ni kuona ligi bora na yenye ushindani mkubwa huku yale makosa ambayo yamekuwa yakionekana uwanjani yakipunguzwa.

Inawezekana ikiwa kila mmoja ataamua kutimiza wajibu wake maana suala la kushindwa kutoa maamuzi sahihi linawamuza wengi.

Kuanzia wachezaji wanaowekeza nguvu kwenye kusaka ushindi pamoja na mashabiki wanaojitokeza kuzipa nguvu timu zao.

Wakati uliopo kwa sasa ni muhimu kufanya maboresho kwenye utendaji na kupunguza yale makosa ya mara kwa mara ambayo yanawezekana kabisa kuwekwa kando.