KLOPP ANACHEKA ISHU YA USAJILI WA JUDE

KOCHA Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp alicheka alipoulizwa kama Liverpool inaweza kumsajili Jude Bellingham mnamo Januari lakini alikiri kuwa klabu hiyo imejiandaa kwa dirisha lijalo la usajili.

Liverpool wamekuwa wakihusishwa na kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Jude Bellingham ili kuimarisha safu yao ya kati ambayo ubora wake umeporomoka kutokana na kuwa na wachezaji ambao umri umekuwa mkubwa.

Lakini alipoulizwa kama dili lolote kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 litalazimika kufanywa tu msimu wa joto badala ya mwezi ujao, Klopp alicheka: “Mwezi Januari? Mimi si mtu sahihi kujibu hilo.”

Hata hivyo, bosi huyo alifichua kuwa klabu hiyo iko tayari kwa dirisha la Januari kufunguliwa.

“Januari, kwa hali yetu, ni dirisha kutoka kwa upande wa michezo ambao tumejitayarisha kila wakati, ni wazi kila wakati tuna mawazo ya aina gani au jinsi hitaji lilivyo kutoka kwa maoni yetu,”

 Liverpool kwa sasa inajiandaa kumenyana na Aston Villa. mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu tangu Kombe la Dunia kugota ukingoni.