KLABU ya Yanga imebainisha kuwa mchezaji Feisal Salum bado ni mali yao na dili lake linagota ukingoni 2024.
Nyota huyo anatajwa kumalizana na mabosi wa Azam FC ambao wameweka dau nono kwa mchezaji huyo.
Yanga wamebainisha kuwa mkwanja ambao alirejesha Feisal wakuvunjia mkataba wake amerudishiwa.
Feisal ameweka wazi kuwa anashukuru kwa muda ambao wamekuwa nao ndani ya Yanga kutokana na kuhudumu kwenye kikosi hicho.