NYOTA wa Yanga Feisal Salum anatajwa kumalizana na mabosi wa Azam FC ambao wanahitaji huduma yake.
Nyota huyo anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Azam FC ambao wanahitaji kuboresha kikosi chao.
Mabosi wa Yanga hivi karibuni waliweka wazi kuwa nyota huyo hawezi kusepa ndani ya kikosi hicho kutokana na mipango iliyopo ndani ya timu hiyo.
Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga alisema kuwa kiungo huyo yupo ndani ya Yanga na hawatarajii kuona akiondoka.
“Feisal yupo ndani ya Yanga kutokana na namna ambayo tumejipanga na kila kitu kinakwenda sawa,” alisema.
Kuhusu suala hilo hivi karibuni Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe alisema kuwa suala la Feisal ni la muda tu.
“Unataka nizungumzie kuhusu Feisal hilo ni suala la muda tu kwani kila kitu kuhusu usajili mashabiki wasiwe na hofu.
“Jambo la msingi ni kutulia na kwenye usajili wetu wa dirisha dogo tunakuja kufagia na kuacha kishindo,” alisema.
Ndani ya Yanga Feisal kafunga mabao sita akiwa ametoa pasi mbili katika mabao hayo mawili aliwatungua Azam FC mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Mkapa.