KLABU ya Manchester United imetinga robo fainali ya Kombe la Carabao kufuatia ushindi wa moja kwa moja wa mabao 2-0 dhidi ya Burnley Uwanja wa Old Trafford.
Bao la Christian Eriksen la kipindi cha kwanza kwa shuti kali kufuatia kazi nzuri ya beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka liliipa United uongozi ilikuwa dakika ya 27.
Juhudi nzuri za pekee kutoka kwa mchezaji aliyekuwa kwenye ubora wake Marcus Rashford mapema katika kipindi cha pili dakika ya 57 lilitosha kuipa ushindi timu hiyo.
Kocha Mkuu wa Manchester United Erik ten Hag alikuwa shuhuda ambapo mchezaji Rashford alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo.